Serikali yaombwa kutenga maeneo mapya kwaajili ya kuzikia

Baadhi ya wakazi wa Kimara jijini Dar es salaam wameiomba Serikali kupitia Mamlaka za Mtaa kutenga upya maeneo ya kuzikia kwa kuwa maeneyo yaliyopo yamejaa, hali inayolazimu kuchimba maeneo yaliyokwishatumika miaka ya nyuma na kuzika upya wafu wengine.

Wakizungumza na channel wakazi hao wamesema kwa sasa heshima ya binadamu inakiukwa kufuatia ufinyu wa maeneo ya kuzikia, ambapo mara kwa mara wachimba makaburi wamekuwa wakikutana na miili ya binadamu iliyozikwa siku nyingi, hivyo kulazimika kuzika mwili mwingine ndani ya kaburi moja.

Akizungumzia changamoto hiyo, Diwani wa Kimara ambako ni miongoni mwa maeneo yaliyoathirika na tatizo hilo, Paschal Manota amesema kimsingi tatizo hilo limekuwa ni sugu katika ameneo mengi.

Aidha, amesisitiza kuwa katika vikao vya baraza la madiwani wa manispaa ya ubungo agenda kubwa itakuwa ni kutafuta fedha kwa ajili kupata maeneo mapya ya kuzikia na kutumia fursa hiyo kutoa rai kwa serikali kutenga fedha kutokana na mapato ya kodi za ardhi ambayo sehemu yake yanarejeshwa kwenye halmashauri.
Mpya zaidi Nzee zaidi