Utaratibu uchangiaji damu kwa wagonjwa hosipitali ya Nachingwea walalamikiwa

Na. Ahmad Mmow.
BAADHI ya wananchi wamelalamikia mfumo wa malipo ya damu wanazochangiwa wa wagonjwa wenye uhitaji wa damu wanaotibiwa katika hospitali ya wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi.

Wakizungumza na Muungwana kwa nyakati na maeneo tofauti wiki hii katika mamlaka ya mji mdogo wa Nachingwea, walisema kiasi cha malipo ya damu kinachotolewa na jamaa za wagonjwa nikikubwa kuliko kiasi wanachopewa wagonjwa kutoka kwenye benki ya damu ya hosipitali hiyo.

Walisema licha ya kiasi kinachofidiwa kuwa kikubwa, lakini pia wachangiaji wamekuwa wakitolewa damu bila kuchukuliwa kwanza sampuli ili kuthibitisha kama damu wanayotoa ni safi au chafu.
                    
Mwajuma Ismaili aliyejitambulisa kuwa nimkazi wa Tunduru ya Leo, mamlaka ya mji  alisema alishangazwa na kitendo cha kutakiwa kufidia uniti(chupa) tatu badala ya moja aliyowekewa mke wa mwanawe ambae  ilitakuwa aongezwe uniti moja.

Licha ya kushangazwa na wingi wa damu ya kulipia, mwananchi huyo alisema alishangazwa zaidi na kitendo cha wiokuwa wanatolewa damu kutolewa bila kuanza kupimwa ubora wake.
"Afadhali sisi ambao wagonjwa wetu walitakiwa kuongezwa chupa moja, kuliko mwenzetu mmoja ambae mgonjwa wake alitakiwa aongezwe chupa tatu, alitakiwa awapeleke watu tisa ili watolewe lita tisa, "alisema Mwajuma. Alitoa

Alitoa wito wachangiaji wapimwe kabla ya kutolewa, ili kuepuka usumbufu wa kuhitajika watu wengi kutolewa damu.7:Maulidi Mohamed wa Mpiruka B, alisema japokuwa serikali inahimiza kujitolea kuchangia damu, lakini ni jambo la hiari. Ambapo mchangani anachangia kiasi anachoweza. Hatahivyo sharti la kutakiwa kufidia kiasi kikubwa kuliko wanachowekewa wagonjwa, sio hiari tena, bali ni lazima. Kwa madai kwamba hakuna ndugu wa mgonjwa anaeweza kukataa, japokuwa atakuwa haridhishwi na utaratibu huo.

"Hivi karibuni nilimpeleka mtoto wa shemeji yangu, alitakiwa aongezwe chupa moja(uniti moja). Hata hivyo niliambiwa niwatafute watu watatu watoe chupa tatu za damu ili kufidia  chupa mmoja aliyopewa mgonjwa wangu. Kibaya zaidi tunachotwa bila damu hiyo kupimwa, ilifaa zichukuliwe sampuli ili mwenye damu chafu asichotwe, "alitoa wito Maulidi.

Bwana  Ismaili Ntila wa Matangani alitoa wito watu wachangie baada ya damu yao kupimwa. Ili ambao damu yao itabainika kuwa hafai wasitolewe. Badala ya mfumo wa sasa ambao unalalamikiwa.
" Hao ambao damu zao ni chafu wangeweza kuelezwa na kupewa ushauri kuhusu matatizo ya kiafya waliyonayo badala ya kutolewa bila kupimwa, sasa huenda ni wagonjwa ndio sababu damu zao mbovu, nawewe ndio umechota damu zao si unakuwa unawaingezea tatizo , "alishuri na kuhoji Ntila.

Mwananchi huyo aliongeza kusema uhenda nia ni njema, hata hivyo kunaumuhimu mkubwa wa kutolewa elimu kuhusu mfumo huo ili kuondoa manung'uniko. Akijibu malalamiko na ushauri wa wananchi hao kwaniaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, na mganga mkuu wa hosipitali hiyo.

Kaimu mganga mkuu, Dkt Ibrahim Pazia, alikiri kuwa katika hosipitali hiyo mfumo wa uchangiaji damu ni wa aina hiyo. Bali ndugu na jamaa za wagonjwa hawalazimishwi kuchangia kabla ya ndugu zao (wagonjwa) kuongezwa damu. Bali wanaongezwa kwa kutumia damu iliyopo kwenye benki ya damu ya hosipitali hiyo.

Dkt Pazia ambae pia ni mganga  mfawidhi wa hosipitali hiyo, alibainisha kwamba damu inayotolewa na wachangiaji hupelekwa Mtwara kwaajili ya kupimwa. Ambapo damu inayobainika kuwa hafai inamwagwa(teketezwa). "Nikweli mgonjwa akiwekewa uniti moja ya damu salama hufidiwa tatu ambazo hupelekwa kupimwa. Huu sio utaratibu uliowekwa na wizara, kwasababu wizara inataka mtu achangie damu kwa kadiri anavyoweza.

Mwanzoni walikuwa  wanatoa sawa na kiasi alichowekewa mgonjwa, hata hivyo damu nyingi baada ya kupimwa zilibainika kuwa ni mbovu. Hivyo kusababisha upungufu kwenye benki ya damu, "alifafanua na kueleza Dkt Pazia. Alisema utaratibu huo umesababisha benki ya damu kuwa na akiba ya kutosha. Kwasababu baada ya kupimwa hupatikana damu salama walau uniti moja au mbili ambazo zinafidia walizopewa wagonjwa.

Kuhusu elimu kwa wananchi, alisema :"Elimu imetolewa kwa kiasi kikubwa, kwasababu wizara inataka kila hosipitali kuwa na mkakati wa ukusanyaji damu ili kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto wa chini ya miaka mitano, "alisema. Mtaalamu huyo aliweka wazi kuwa utaratibu huo uliridhiwa na timu za uendeshaji hosipitali hiyo na huduma za afya ya wilaya (CHMT).

Uchangiaji damu kwa hiari umekuwa ukihimizwa na serikali. Lengo nikuwa na akiba ya kutosha kwenye benki za damu, ili kukabiliana na upungufu unasababisha watu kupotea maisha. Hasa zinapotokea ajali na kusababisha majeruhi wanalohitaji kuongezwa damu haraka.


Mpya zaidi Nzee zaidi