Wazee wapata shida kupiga kura Kenya

Nairobi. Askofu Peter Philip Dungu mwenye umri wa miaka 70 amelala katika kituo cha kupigia kura. Ameiambia MCL kuwa alikuja tangu jana saa mbili na nusu usiku, na kufanikiwa kupiga kura saa mbili asubuhi akiwa mtu wa 20 kufanya hivyo katika kituo chake.                      

Dungu ameisifia Tume Huru ya uchaguzi na Mipaka (IEBC) akisema imeweka utaratibu mzuri na maofisa wake wanafanya kazi vizuri.

Alisema anaamini kwa namna upigaji kura unalivyoanza vizuri pia utamalizika vizuri, kwa kuwa ana uzoefu wa kuona uchaguzi uliopita.

Naye John Ndegwa Kenywa aliyekutwa akisubiri kupiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Moi, alisema alifika kituoni hapo saa 10.30 alfajiri lakini kutokana na msongamano wa watu, ameamua kusubiri pembeni kwanza. Kenywa ana umri wa miaka 52.

Kenywa alisema anaamini atapiga kura kwa kuwa mstari wake tayari ameuona.

Akizungumza na mwandishi saa 2.30 asubuhi, Kenywa alisema utaratibu wa mwaka huu ni mzuri kwa kuwa idadi ya vituo imeongezwa.

Hata hivyo, kuna watu wengi ambao bado hawajafahamu mahali wanapopaswa kupigia kura.

Baadhi ya watu walituma SMS kujua wako mstari gani, lakini walisema wamesubiri kwa muda mrefu hakuna ujumbe ulioingia kuwaeleza wasimame mstari upigaji.

Thomas Obiero alifika kituoni saa moja asubuhi na hadi saa mbili na nusu alikuwa hajajua anapaswa kuwa katika mstari gani.

Alisema utaratibu huu ni mbovu kwa sababu watu kama wazee au wasio na simu watajuaje mstari wanaotakiwa kusimama ili wapige kura.

Thomas amesema utaratibu wa zamani wa alphabet ulikuwa mzuri kwa kuwa mtu unaangalia herufi ya jina lako unajipanga.Amesema utaratibu huu utasabasha kuchelewa kwa watu kupiga kura.

Naye Zebidah Kamau mama ambaye ni mtu mzima kidogo amesema amejaribu kutuma ujumbe kwenye namba aliyoambiwa lakini unamletea ujumbe kwamba amekosea.

Zebidah anayepiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Moi alisema tatizo lingine maofisa wa IEBC hawaonekani nje kwa ajili ya kuwasaidia zaidi ya polisi ambao wako kwa ajili kuwapanga vizuri Watu wasiruke foleni.

Hali ya mvua hapa katika jiji la Nairobi ni ya manyunyu na baridi karidi, mitaa yote iko tupu, hasa mitaa wa Thom Mboya ambao ni maarufu kwa wingi wa watu leo uko kama mtupuWazee ni miongoni mwa waliodamka usiku wa manane, washangaa utaratibu wa sasa siyo mzuri washindwa kusimama kwenye mstari
Mpya zaidi Nzee zaidi