Dkt Kigwangala asitisha ziara ghafla,"achimba mkwara mzito" kwa viongozi na watendaji wa wilaya ya Lindi.

Na.Ahmad Mmow.
NAIBU waziri wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto,Dkt Hamisi Kigwangala ,leo amesitisha ghafla ziara yake katika wilaya ya Lindi.Kwamadai ya kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi na watendaji wa wilaya hiyo.

Dkt Kigwangala ambae kabla ya kusitisha ziara katika wilaya hiyo alikwenda na kutembelea kituo cha afya cha Rutamba alisema alilazimika kusitisha ziara baada ya kuona kwenye msafara wake kutokuwepo viongozi na watendaji wa wilaya hiyo ya Lindi.Kwahiyo hakuona sababu ya kuendelea na ziara ambayo ingefanana na utalii.Huku akibainisha kwamba watendaji na viongozi hao wangekuwepo wangepokea maelekezo na hata kushauriana nae.

Naibu waziri huyo akionesha dhahiri kuchukizwa na kitendo hicho alisema wakurugenzi wa halmshauri ni watekelezaji wa sera,na wakuu wa wilaya ni wasimamizi wa utekelezaji.Hivyo kitendo cha kushindwa kutoa ushirikiano kwake ni ushahidi kuwa wameshindwa kwenda na kasi ya awamu ya tano.Nakuongeza kusema kuwa kitendo hicho kinadhihirisha viongozi na watendaji hao wamachoka.Hivyo yeye akirudi wizarani atawaandikia barua wenye mamlaka ya uteuzi kueleza jinsi viongozi na watendaji wa ngazi za chini wanavyoshindwa kuendana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.

Alisema ni jambo la kusikitisha kuona eneo ambalo linachangamoto zinazohitaji utatuzi wa pamoja,viongozi na watendaji wake wanashindwa kutoa ushirikiano na viongozi wakitaifa ambao wanakwenda kwania njema kwa masilahi ya wananchi.

"Nikirudi ofisini nitaandika dokezo kwa wenye mamlaka nakuwaeleza kwamba hao waliowateuwa huku chini wamechoka,ili waweze kuchukua hatua.Nilitaraji wote tungekwenda nakasi inayofanana lakini wenzetu wamechoka," alisema Dkt Kigwangala.

Naibu waziri huyo kijana alikwenda mbali zaidi nakusema mkoa wa Lindi nimiongoni mwa mikoa yenye changamoto nyingi katika sekta ya afya. Hata hivyo kitendo kilichofanywa na viongozi na watendaji hao kinaonesha kutojali hali hiyo.

Huku akiongeza kusema "Maagizo mengi hayajatekelezwa katika mkoa huu,tuliagiza hadi kufikia mwezi Juni tarehe 30 mwaka huu vituo vya afya viwe na maabara na vyumba vya upasuaji kwa akina mama wajawazito,lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika.Nimiezi mitatu toka tarehe ya mwisho. Nimetetembelea mikoa mingi tu lakini sijapata ushirikiano hafifu kama niliopata katika mkoa huu," alifafanua na kusikitika Dkt Kigwangala.

Alipoulizwa kuhusu malalamiko na madai ya naibu Waziri huyo,mkuu  wa wilaya ya Lindi,Shaibu Ndemanga, licha ya kumpongeza naibu Waziri huyo kwa uchapaji kazi,moyo wa kujitolea na kitendo chake cha kufanya ziara katika wilaya hiyo,alisema hali iliyojitokeza ilisababishwa na mabadiliko ya ratiba ya naibu waziri huyo.

Ndemanga alisema nijambo lisilowezekana apuuze na kudharau ziara hiyo.Bali awali ilielezwa angefanya ziara katika wilaya za Ruangwa,Nachingwea na Liwale pekee.Hata hivyo ghafla alisikia kuwa anafanya ziara katika wilaya yake. "Nimekuja kuonana nae nimetoka kwa mkuu wa mkoa kuthibitisha.Pia tukumbuke tulikuwa na maandalizi na mapokezi ya waziri mkuu.Nalo limechangia kutopatikana mawasiliano ya mabadiliko ya ratiba kwa wakati, "Ndemanga alisema kwa unyonge na huzuni.

Naibu Waziri huyo anaendelea na ziara katika wilaya nyingine za mkoa huu wa Lindi.Ambapo kesho ataendelea na kuanza katika wilaya ya Ruangwa.


Mpya zaidi Nzee zaidi