Msuva afunguka kuhusu hili

Winga wa klabu ya Difaa El Jadida na timu ya taifa ya soka ya Tanzania Simon Msuva amefunguka kuhusu mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars dhidi ya Malawi.

Akiongelea mchezo huo utakaopigwa Jumamosi ya Oktoba 7 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Msuva amesema kuwa wana matumaini kuwa wataibuka na ushindi.

“Mechi ya Jumamosi dhidi ya Malawi itakuwa nzuri na tunaamini tutashinda kama tulivyoshinda mechi ya awali na Watanzania watafurahi”, amesema Msuva.

Aidha Msuva ambaye yupo kambini na timu ya taifa amewataka mashabiki wa soka nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwapa hamasa wakati wa mchezo.

Taifa Stars na Malawi zilikutana miezi miwili iliyopita kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika Kusini ambapo Stars ilishinda mabao 2-0.

Mpya zaidi Nzee zaidi