Arusha. Mdau wa michezo Mwigulu Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, atakuwa kwenye kipindi kigumu wakati timu ya Yanga itakapokutana na Singida United keshokutwa Jumamosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu.
Mchuano huo wa kukata na shoka, utakuwa mgumu kwa Nchemba kutokana na mahaba aliyonayo dhidi ya timu hizo mbili zinazokutana.
Wakati nyasi za Uwanja wa Namfua zikiwaka moto dhidi ya mahasimu hao wawili walioonja ufundi wa kocha Hans Pluijm, ndivyo mapigo ya moyo ya mbunge huyo wa Iramba yatakavyokuwa juu siku hiyo.
Nchemba si mara moja ameonekana katika mahaba mazito na timu ya Singida United hasa kujitolea michango yake kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri, lakini ndivyo ilivyo kwa klabu yake ya Yanga, ambayo amekuwa akijitokeza mara kwa mara kuishuhudia ikipambana na timu zingine.