Simba kuifuata Mbeya City kwa ndege kesho

TIMU ya Simba inatarajiwa kusafiri kesho Ijumaa saa tatu kamili asubuhi kwa njia ya ndege kuwafuata wapinzani wao Mbeya City kwa ndege.

Simba itaelekea mkoani Mbeya kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Jumapili ya wiki hii kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani huko.

Katika mechi hiyo, Simba itavaana na Mbeya ikiwa na hasira ya kuzikosa pointi tatu za mechi iliyopita dhidi ya Yanga.

Akizungumza na Salehjembe, Mratibu wa timu hiyo, Abbas Ally alisema taratibu zote za kukamirisha safari hiyo zimekamilika.

“Timu inatarajiwa kuondoka jijini Dar kesho saa tatu kamili asubuhi na ndege tukielekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Mbeya City.
“Tutakuwa tukiwa hatuna majeruhi yeyote katika kikosi chetu, hivyo ni jambo jema kwetu katika kufanikisha pointi tatu katika mchezo wetu huu muhimu,”alisema Ally
Mpya zaidi Nzee zaidi