Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge amewaambia wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutohamaki kuhusu bomoabomoa inayoendelea katika manispaa ya Dodoma kwa sababu inalenga kuleta maendeleo.
Dk Mahenge ametoa kauli hiyo leo wakati akiwasilisha taarifa ya mkoa kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Mkoa wa Dodoma ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya uchaguzi.
Juzi na jana kulikuwa na vilio kwa wafanyabiashara wa manispaa ya Dodoma katika Marnie ya soko la Sarafina na stand ya mkoa baada ya mabanda yao kuvunjwa katika maeneo yanayotajwa ni ya shirika la Reli.
Mahenge amesema kila jambo jema lazima linakuwa na changamoto zake na ujenzi wa reli ya standard Gage nao umekuja na changamoto zake.
"Mheshimiwa Rais alishasaini mkataba wa ujenzi wa reli hiyo kwa awamu ya kwanza na wakati wowote atasaini awamu ya pili toka Morogoro kuja Dodoma, lazima tukubali kuanza maandalizi yake," amesema Mahenge.
Mkuu huyo aliwaagiza wanachama hao kuwa mfano bora katika matendo ikiwemo suala la elimu na kilimo ili kuondoa mtazamo hasi kuwa watu wa Dodoma ni ombaomba.
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Adam Kimbisa amewataka wajumbe wa mkutano kukubali kuwa makao makuu yaliyopelekwa mkoani hapo yatakuwa na changamoto pia.
Kimbisa amesema ujio wa wageni utakuwa ni chachu ya maendeleo hivyo wananchi wasikubali kupitwa na fursa hizo ikiwemo kuongeza zaidi kasi ya kilimo na kusomesha watoto wao ili wawe na uwezo wa kupambanua mambo ya kimaendeleo.
Msimamizi wa uchaguzi huo Subira Mgalu amewataka wajumbe kuwa na uamuzi sahihi na waache kusikiliza kelele za wapambe wa nje.
Mgalu ametangaza idadi ya wajumbe waliotakiwa kupiga kura kwamba walikuwa 1233 lakini hadi wanaanza upigaji kura kulikuwa na wajumbe 1104