Na. Ahmad Mmow.
WAKULIMA wa korosho nchini wameshauriwa kujiandaa kununua pembejeo kwa ajili ya msimu ujao badala ya kutegemea pembejeo za bure kutoka serikalini.
Wito huo ulitolewa jana na meneja rasilimali watu na utawala wa bodi ya korosho nchini(CBT) , Shauri Mokiwa, wakati wa ufunguzi wa zabuni za ununuzi wa korosho za wakulima waliopo katika chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao, uliofanyika katika kijiji cha Navanga, wilaya na mkoa wa Lindi.
Mokiwa ambae aliyasema hayo kufuatia swali la mkulima, Ahmad Kimbiu aliyetaka kujua kama serikali itatoa pembejeo za bure kwa wakulima wa korosho msimu ujao ama la, alisema wakulima wa zao hilo hawana budi kutenga fedha kwa ajili ya kununuulia pembejeo badala ya kutegemea pembejeo za bure kutoka serikalini.
Alisema hakuna uhakika kama serikali katika msimu ujao itatoa tena pembejeo na kuzigawa kwa wakulima kama msimu huu. Kwani mpaka sasa haijatangaza kuendelea na mpango huo katika msimu ujao wa 2018 /2019.
"Ninachoweza kuwana na uhakika nacho ni pembejeo za ruzuku, hizo, zinaweza kuwepo. Lakini pembejeo za bure siwezi kuwahakikishia. Kwahiyo jiandaeni kununua pembejeo," alisema.,"alisema Mokiwa.
Mbali na hilo, ofisa huyo wa bodi ya korosho alikubali kuuchukua na kuufanyia kazi ushauri wa mkulima Issa Kitenge, ambae alishauri msimu wa ununuzi wa zao hilo ufunguliwe mapema kuanzia mwezi Agosti au Septemba ili kuzuia wakulima wasiuze kwa walanguzi.
Mokiwa alisema ushauri wa mkulima huyo ni wa msingi, hivyo bodi kwa niaba ya serikali imepokea na itaufanyia kazi kwa masilahi mapana ya wakulima na uchumi wa taifa.
Katika mnada huo bei ya juu ya kilo moja ya korosho ghafi za daraja la kwanza iliuzwa na kununuliwa kwa shilingi 3760. Ambapo bei ya chini ilikuwa shilingi 3700.
Kwa mujibu wa meneja mkuu wa Lindi Mwambao, Hassan Vudu, kampuni kumi ndizo zilizotuma maombi. Ambapo barua 11 zilisomwa.
" Mnada uliopita kulikuwa na kampuni 22, lakini mnada wa leo ni kampuni kumi tu, hali sio mzuri, "alisema Vudu.
Nae ofisa maendeleo ya ushirika toka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Lindi, Robert Nsunza alizitaja kampuni zilizoshinda mnada huo kuwa ni Africian Ltd (tani 200), RCN Tanzania Ltd (tani 147),Agro Company Ltd (tani 470),OM Agro (tani 200) na Thabit Export (100)