Waziri wa Nishati, Medard Kalemani ameiomba wizara ya ujenzi kuharakisha mchakato ujenzi wa flow mita katika bandari ya Tanga ili ziweze kutumika kudhibiti uingizaji wa mafuta nchini. Kauli hiyo ameitoa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika bohari ya Gbp jijini hapa ili kujiridhisha na utaratibu wa uingizaji mafuta katika bandari ya tanga
Amesema kukamilika kwa ufungaji wa flow mita kutaiwezesha serikali kuhakiki kiwango cha mafuta yanayoingia nchinikupitia bandari ya tanga na kuondoa uwezekano kufanyika udanganyifu.
Awali akizungumza katika ziara hiyo mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela ameishukuru serikali kwa kukubali ombi la kupanga bei tofauti ya mafuta yanayoshushwa katika bandari ya Tanga.
kwa upande wake meneja wa bohari ya GBP Amour Ally amesema upanuzi wa bohari hiyo utawezesha kuongeza ufanisi katika upakiaji kutoka magari 2 hadi 12 na mabehewa 3 hadi 20 kwa wakati mmoja.
Katika ziara hiyo Waziri Kalemani ametembelea kituo cha kupozea umeme cha majani mapana na kulitaka shirika la umeme kukamilisha haraka ufungaji wa transfoma .