KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, George Lwandamina, amekiri mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC utakuwa mgumu kwa kutokana na kukosekana kwa baadhi ya nyota wake wa kikosi cha kwanza. KOCHA Mkuu wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, George Lwandamina,
Yanga ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Sportpesa, leo inawafuata mabingwa wa Kombe la Mapinduzi katika mchezo wa ligi hiyo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Azam bila ya mshambuliaji wake, Amissi Tambwe, Thaban Kamusoko, Pius Buswita na Pato Ngonyani.
Tambwe ambaye alianza mazoezi na timu yake wiki hii, juzi alijitonesha tena kwenye mguu wake na hivyo atakosekana katika mchezo wa leo ambao unakamilisha mzunguko wa kwanza.
Akizungumza na Nipashe jana, Lwandamina, alisema wanatarajia kukutana na ushindani na anauona mchezo wa leo kuwa ni mgumu, lakini kama timu imejiandaa kupambana kwa ajili ya kuvuna pointi tatu.
“Hatutakuwa na Tambwe, Buswita pia Kamusoko naye hajawa fiti, lakini tutapambana, tunawaheshimu Azam lakini hatuwahofii,” alisema Lwandamina.
Kukosekana kwa Buswita, bado kunamfanya Mzambia huyo kumpanga Raphael Daudi au Saidi Makapu kwenye kiungo, atakayecheza pamoja na mkongo Papy Tshishimbi.
Kwa upande wake, Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba, alisema kuwa atatumia udhaifu aliouona kwenye kikosi cha Yanga kuweza kupata ushindi kwenye mchezo huo ambao unahusisha timu zinazowania ubingwa.
“Nina kikosi imara, tupo tayari kukabiliana na Yanga na sina shaka, Yanga ni timu kubwa, lakini hilo halitusumbui kwa sababu mpira unachezwa uwanjani, tusubiri dakika 90,” alisema kocha huyo.
Nkongo kusimama katikati
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa refa, Israel Nkongo, atachezesha mchezo huo kutokana na uzoefu ambao anao wa mechi za Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa licha ya wenyeji Azam kuwasilisha barua ya kutokuwa na imani na mwamuzi huyo.