Wafuasi sita wa kundi la Musilim Brotherhood lililopigwa marufuku nchini Misri wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kupanga kufanya vurugu ili kuvuruga uchaguzi wa rais utakaofanyika Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo watu hao walikamatwa katika misako miwili tofauti iliyofanywa na polisi.
Misri ilitangaza kundi hilo la Muslim Brotherhood ni mtandao wa kigaidi baada ya jeshi kufanya mapinduzi mwaka 2013 yaliyomuondoa madarakani rais wa kwanza nchini humo kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia Mohammed Morsi.