Na. Ahmad Mmow.
MAZAO ya a misitu na bidhaa za viwandani zimekamatwa wilayani Kilwa mkoa wa Lindi, kufuatia msako mkali ulioongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Christopher Ngubiagai.
Akizungumza na Muungwana kutoka katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko kuhusu tukio hilo, Ngubiagai alisema msako huo ulioratibiwa, kusimamiwa na kutekelezwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo umewezesha kukamatwa jahazi mbili. Ikiwamo moja iliyosajiliwa na yenye jina la Hadija, zikiwa zimepakiwa mazao ya misitu na bidhaa za viwandani, tayari kwa kusafirishwa zikiwa hazijalipiwa ushuru wala kodi.
Alisema Hadija ilikutwa imepakiwa vipande 560 vya mbao. Huku jahazi jingine ambalo halijasajiliwa na halina jina, lilikutwa na bidhaa za viwandani.
Mkuu huyo wa wilaya alisema licha ya kukamata bidhaa hizo ndani ya vyombo vya kusafiria baharini, lakini pia msako huo ulifanikisha kukamatwa vipande 828 vilivyokutwa vimehifadhiwa ndani ya nyumba ya kuishi ya mwananchi mmoja ambae amekimbia nakwenda mahali kusikojulikana.
"Pamoja na hayo tumekamata gari ambayo bila shaka ilikuwa inapeleka bidhaa kwenye bandari bubu. Ikiwa imepakiwa vipande vinne vya mbao na gunia kumi na tano za mkaa," alisema Ngubiagai.
Mwenyekiti huyo wakamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kilwa alisema jumla ya mbao zote zilizokamatwa ni vipande 1388 ambazo kama zisingekamatwa, ushuru wenye jumla ya shilingi 27,577,700.40 zingepotea, Huku akiweka wazi kwamba bidhaa nyingine zilizokamatwa kwenye bandari bubu ya Milamba kuwa ni mafuta ya kula ndoo 383, sabuni ya unga mifuko 76 yenye uzito wa kilo 112 na televisheni mbili aina ya Philips zilizotengenezwa Uingereza. Bidhaa ambazo zingeweza kupoteza ushuru wa shilingi 19044, ambazo pia zingisababisha serikali ikose shilingi 13, 261,631. 12 iwapo zisingekatwa.
"Utaona kuwa bidhaa za viwandani na mazao ya misitu yangetoroshwa na hao akina Hadija serikali ingepoteza takribni shilingi milioni hamsini,nahuyo aliyekimbia bila shaka kwa sheria za sasa nyumba yake hiyo inaweza kutaifishwa, "alichekesha na kufafanua Ngubiagai.
Mbali na hayo mkuu huyo wa wilaya aliongeza kusema atawaita viongozi na watendaji ambao maeneo yao ya utawala zimekamatwa bidhaa na mazao hayo ya misitu.
Lengo likiwa ni kujua jinsi wanavyoshiriki kudhibiti usafirishaji bidhaa na mazao ya misitukwa njia za magendo na namna wanavyokabiliana na uvuvi haramu na uharibifu wa misitu.
Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa wilaya zilizo katila changamoto kubwa ya uvuvi haramu, bandari bubu na uharibifu wa misitu. Huku ikionesha juhudi za kupambana na uvuvi haramu zimeanza kuzaa matunda Kutona na kuongezeka kwa kasi upatikanaji wa samaki katika kipindi cha karibuni baada ya kuwepo misako na doria za mara kwa mara.