Mtoto afariki wakati akitolewa mapepo

KAMANDA WA POLISI MKOA WA GEITA, MPONJOLI MWABULAMBO.

Mtoto wa miaka 6 amefariki dunia mkoani Geita wakati akiombewa mlimani alikopelekwa kutolewa mapepo, huku mama yake mzazi akishikiliwa polisi.

Akithibitisha kutokea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema tukio hilo lilitokea Februari 18,2018 saa tano asubuhi katika mlima Gambiwe, ambapo mtoto huyo alipelekwa kwa jali ya kuombewa ili kutolewa mapepo.

Amesema mama wa mtoto Neema Petro (25) na mke mwenzake Raheli Musa (25) walikwenda mlimani na mtoto huyo kwa ajili ya maombi na kufunga.

Kamanda i Mwabulambo, amesema wanawake hao wakazi wa kijiji cha Bukulu wilayani Nyang'hwale wanashikiliwa kutokana na kifo cha mtoto Frank Bariki (6), ambaye mwili wake umekutwa na majeraha shingoni na kwenye mbavu.
Mpya zaidi Nzee zaidi

Popular Items