Viongozi wa chama cha Ukombozi wa Palestina PLO, jana wameiamuru serikali ya Palestina kuanza mara moja mipango ya kutengana na Israeli katika ngazi zote.
Uamuzi huo umetolewa katika mkutano wa kamati kuu ya utendaji ya chama cha PLO uliofanyika Ramallah na mwenyekiti wake akiwa Rais Mahmoud Abbas.
Wito wa kutengana na Israel ulianza baada ya Marekani kutangaza kuitambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel mnamo Desemba 6, hatua iliyopelekea Abbas na Mamlaka ya Palestina kutangaza kwamba Marekani haiwezi tena kuwa mpatanishi wa kuaminika katika mazungumzo ya amani na Israeli.