Papa Francis atoa wito wa kusitiswa mapigano Syria

Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Papa Francis atoa wito wa kusitishwa kwa mapigano  nchini Syria ili kurahisisha  misaada ya kiutu kuingia.

Papa Francis akiongea na  raia San Pietro  Vatican  amezungumzia hali inaypoendelea nchini Syria ametoa wito wa kusitishwa mapigano na kuruhusu kuingia maisaada ya kiutu.

Miaka 7 imetimia tangu kuanza kwa mapigano nchini Syria na kuwaacha raia katika hali ngumu.

Mashambulizi ya anga yanayotekelezwa Ghuta na maeneo mengine yanazidi kuhatarisha maisha ya raia nchini Syria ambao tayari wameathirika na uhaba wa chakula na madawa.
Mpya zaidi Nzee zaidi