Rais wa ANC Cyril Ramaphosa amewasili kwenye makazi rasmi ya Rais Jacob Zuma leo mchana saa chache baada ya Zuma kulihutubia taifa kupitia mahojiano aliyofanya na shirika la utangazaji la SABC.
Msafara wa Ramahosa ulikuwa wa magari manane na waliwasili kwenye makazi yake rasmi ya Mahlamba Ndlopfu bila ving’ora wala taa za blu. Ajenda ya mazungumzo yao baada ya kufika haikujulikana.
Katika mahojiano na SABC, Zuma alionyesha kwamba atatoa taarifa ya maandishi baadaye leo kuhusu uamuzi wa chama chake kutaka ajiuzulu.
Ramaphosa anapigiwa upatu kwamba anaweza kuteuliwa na Bunge kesho na kuapishwa kesho hiyo hiyo au Ijumaa.
"Sasa tumemtaka mnadhimu mkuu wa chama kuendelea na uwasilishaji wa hoja bungeni ya kutokuwa na Imani kesho (leo) bungeni ... ili Rais Zuma aondolewe rasmi," alisema mweka hazina mkuu wa ANC Paul Mashatile alipozungumza na waandishi wa habari Jumatano.
Alisema bunge, ambalo lina wabunge wengi wa ANC "litasonga mbele kumchagua (Cyril) Ramaphosa kama rais wa jamhuri" - labda mapema asubuhi leo au kesho Ijumaa.