Mnamo February saba mwaka huu wakurugenzi wa halmashauri za wilaya ya masasi mkoani Mtwara kwa kutii agizo la mkuu wa mkoa waliunda tume ya kuchunguza madai ya wakulima wa zao la korosho wilayani humo ambao wanadai fedha zao za msimu wa mwaka 2016/2017 pamoja na msimu wa mwaka 2017/2018.
Siku kumi na sita baadae tume hiyo inawasilisha report ya uchunguchi kwa mkuu wa mkoa na hapa mwenyekiti wa tume Remidius Bantulaki anabainasha madai ya wakulima.
Mkuu wa Mkoa Gelasius Byakanwa anakubaliana na mapendekezo yote ya tume juu ya wahusika na kuagiza.
Meneja wa benki ya NMB wilaya ya Masasi anawekwa chini ya ulinzi kutokana na kutokuhamisha fedha za wakulima kutoka benki yake kwenda benki ya CRDB ambako kuna akaundi za wakulima mmoja mmoja huku akikopesha shilingi milioni mia tatu chama cha msingi bila chama kuomba.
