Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Zimbabwe, Profesa Levi Nyagura, Ijumaa usiku alikamatwa na Tume ya Kupambana na Ufisadi (ZACC) akituhumiwa kumtunukia shahada ya uzamili (PhD) Grace Mugabe.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Nyagura anadaiwa kuwa "alipendekeza bila idhini ya baraza la chuo kikuu" kwamba mke huyo wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe atunukiwe shahada hiyo.
Msemaji wa ZACC Phyllis Chikundura alisema msomi huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumamosi asubuhi.
"Yuko kizuizini. Atafikishwa mahakamani kesho (leo) kukabili mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi," alisema.
Idara ya sosholojia ya chuo hicho iliwasilisha Januari malalamiko kwa ZACC ikitaka ifuatilie suala hilo, ambalo walielezea kuwa ni la kushangaza.
Robert na Grace Mugabe wanaishi kwa furaha lakini mwanamke huyo anaweza kushtakiwa kwa uhalifu anaodaiwa alifanya wakati mumewe alipokuwa madarakani.
Malalamiko hayo ni kwamba tuzo hiyo "iliwashtua wasomi wengi wa idara" na kwamba wanachama wengi walisikia tu kuhusu uhitimu wa Mugabe katika vyombo vya habari na waliona picha katika kalenda ya chuo kikuu. Waliongeza kuwa wafanyakazi wa idara hawakuwahi kuona pendekezo la utafiti la Mugabe, mchakato wa ripoti au matokeo ya utafiti wowote.
Wakati ule, ZACC ilitoa taarifa ikisema imepokea malalamiko lakini haikufuatilia jambo hilo.
Miaka minne tangu alipotunukiwa shahada hiyo mwaka 2014, haikuonekana kwa urahisi kwenye tovuti ya chuo kikuu. Iliwekwa mtandaoni mwishoni mwa Januari mwaka huu.
Nyagura alidai kuwa ilikuwa inapatikana kwenye maktaba ya chuo kikuu, na aliwaonya wahadhiri aliodai walikuwa "hawajui taratibu za chuo kikuu".
Nyaraka hizo zenye kichwa “Mabadiliko ya Mfumo wa Jamii na Shughuli za Familia: Maisha ya Watoto katika Nyumba ya Kulelea Zimbabwe” zilipowekwa mtandaoni, baadhi ya wahadhiri walisema ulikuwa sawa na udanganyifu wa kitaaluma na wala haikustahili kuitwa kuwa utafiti wa shahada ya kwanza.