Baada ya kukamilika kwa taarifa ya malalamiko ya Wananchi, jopo la Wanasheria na wataalamu zaidi ya 100 wameanza kufanya uchambuzi wa kutoa majibu ikiwemo kuwaita Walalamikiwa ambao mashauri yao hayapo kwenye ngazi ya Mahakamana ili kumshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda juu ya hatua za kuchukuwa ili haki ya Mnyonge ipatikane pasipokuvunja Sheria.
 |
| Mwanasheria wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Fabiola Mwingira |
Mwanasheria wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Fabiola Mwingira amesema kuwa jopo hilo la Wanasheria na Wataalamu litafanya uchambuzi kuanzia leo February 26 hadi ijumaa ya March 09 hii yote ni kuhakikisha kila mwananchi alieleta malalamiko anapatiwa majibu kwa wakati.
Aidha Bi. Fabiola amesema kuwa tayari Wananchi waliokuwa wakihitaji Msaada wa kisheria wamepatiwa msaada huo kwa kufikishwa kwa wadau wanaotoa msaada wa kisheria na wale ambao kesi zao zilikuwa zikiendelea Mahakamani wameandikiwa barua za moja kwa moja waendelee na kesi zao ili kuepuka kuingilia Uhuru wa mahakama.