Aubameyang alabata na mtoto wa Beckham


Mchezaji wa klabu ya Arsenal, Pierre – Emerick Aubameyang ameutumia usiku wake wa jana kula raha na mtoto wa mcheza soka wazamani wa Manchester United, David Beckham baada ya timu yake kufanikiwa kuitoa AC Milan katika michuano ya Europa League na kutinga hatua ya robo fainali.

Mtoto huyo wakiume wa David na mkewe Victoria Beckham alitupia picha katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram zikionyesha wakiwa pamoja na Auba.


The Gunners inarejea Uingereza huku ikiwa na jukumu moja tu lakuwaalika Stoke City mwezi Aprili baada ya mapumziko yao ya mchezo wa kimataifa.

Aubameyang ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Gabon, ameisaidia timu yake ya Arsenal baada ya kusajiliwa akitokea Borussia Dortmund kabla ya msimu wa mwezi Januari.