Wahamiaji haramu 34 raia wa Burundi wakamatwa Uvinza


Na. Mwandishi wetu, Kigoma.

‎Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Uvinza, Kanda Maalumu ya ki-Uhamiaji Kigoma imewakamata Wahamiaji haramu 32 raia wa Burundi  walioingia Nchini Kinyume Cha Sheria.

‎Ukamataji huo imefanyika  leo, Oktoba 07  2026, katika Kizuizi cha Kibaoni , kilichopo Kata ya Uvinza Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.

‎Zoezi hilo liliongozwa na Sajinitaji  wa Uhamiaji Bashiru Ntandu ambapo watuhumiwa hao walikutwa wakijihusisha na shughuli za kilimo na kuhudumia katika baa kinyume cha Sheria.

‎Akizungumza baada ya zoezi hilo, Afisa Uhamiaji wilaya SI Kivelia Lema amesema watuhumiwa wanaendelea kuhojiwa na baada ya kukamilika kwa taratibu watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili na kwa wale walio chini ya Miaka 18 watapatiwa elimu ya uhamiaji  na kuondoshwa nchini kwao kwa utaratibu

‎SI Lema amesisitiza kuwa Ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya Uvinza itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi