Bale ataja hiki ndio kitu muhimu kwake


Nyota wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales Gareth Bale amesema kwasasa kitu muhimu kwake ni kuchukua vikombe akiwa na timu yake ya taifa, ambayo kwasasa inafundishwa na Ryan Giggs.

Bale anatarajia kucheza mchezo wa fainali wa Kombe la China leo dhidi ya Uruguay baada ya kutinga fainali juzi kwa kuifunga China mabao 6-0 ambapo Bale alifunga Hat-trick na kuwa mfungaji kinara wa muda wote wa taifa hilo.

"Kushinda vikombe daima ni kitu kizuri, lakini kushinda kweney timu ya taifa ya ni nzuri  na maalum zaidi," amesema Bale ambaye klabu yake ya Real Madrid haina msimu mzuri sana kutokana na kutofanya vizuri kwenye La Liga pamoja na Copa del Rey.

Bale mwenye miaka 28 amefikisha mabao 29 katika 69 alizoichezea Wales toka mwaka 2006 na kumzidi nyota wa zamani wa taifa hilo Ian Rush mwenye mabao 28 katika mechi 73 na aliichezea Wales toka mwaka 1980 hadi 1996.
Mpya zaidi Nzee zaidi