Mambo Matatu Ya Yuyaepuka Katika Safari Yako Ya Mafanikio

Kuna wakati umekuwa unajilaumu kwamba maisha yamekuwa ni magumu, pengine husema umelogwa, hata kudiriki kusema huna bahati na meneno mengine kama hayo.  Hizo na sababu zinginezo ni woga binafsi ambao kimsingi kama utaendelea kuzibeba basi kufanikiwa kwako itakuwa ni ngumu.

Nilichigundua ni kwamba watu wengi tunashindwa kufanikiwa kwa sababu ya mambo haya;

1.Kusubiri mtu mwingine akufanyie maamuzi.
kama tulivyosema hapo awali ya kwamba maisha  yako yapo mikononi mwako kwanini uache mtu mwingine afanye maamuzi juu ya maisha yako? Najaribu kuwaza kwa sauti ila sipati majibu.
Nasema hivyo kwa sababu maisha yetu yanakuwa ya kawaida kwa sababu tunapenda kuwaruhusu watu wengine watoe maaumuzi katika kutenda jambo fulani.

Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kufanikiwa jaribu kutafakari juu ya maisha yako na uamue kutoa maaumuzi juu ya jambo hilo. Lakini pia baada ya kutafakari ni nini cha kufanya jambo la msingi ni kuhakikisha unapata mtu sahihi wa kukushauri ni nini ufanye katika jambo hilo ili uwe bora zaidi.

2. Kukata tamaa mapema.
Watu wengi sana huwa tunaathiriwa na ugonjwa huu wa ukataji tama mapema, na hii ni kwasababu wengi wengi wetu huwa tunapenda matikea ya papo kwa papo. Ila ukweli ni kwamba mafanikio ya papo kwa papo hakuna labda uamue kucheza bahati nasibu. Ila kama unataka matokeo ya uhakika na yenye kuleta mafanikio ya kweli unachokihitaji ni kuwa mvumilivu kwa kila hatua ambayo unapiga kila siku katika jambo ambalo unalolifanya.

Hivyo niweke nukta katika maelezo haya kwa kusema ya kwamba kuwa mvumilivu kila wakati. Kwani mvulivu hala mbivu, ila  kumbuka kuongeza hatua za kiutendeji ambazo zitakufanya uweze kusonga mbele na si kukata tamaa. Kwani kukata tamaa ni chukizo mbele za Mungu wetu.

3. Kuridhika mapema.
Kuridhika mapema ni adui mkubwa wa mafanikio yako, naomba hili libaki kichwani mwako. Mafanikio hayana ukomo, kila siku na kila wakati ona kabisa bado hujafanikiwa hata kama watu wanasema umefanikiwa. Usibweteke na hali uliyonayo. Daima kumbuka ya kwamba "Mafanikio ni njaa isiyoisha" hivyo kuridhika ni kurudi nyuma katika hali ya kiutendeji.

Nimalizie kwa kusema tena mafanikio hayana ukomo, hivyo achana na tabia ya kuridhika mapema.