Na James Timber, Mwanza
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameipongeza Kamati ya Utafiti wa Madini kupendekeza soko la madini liwepo katika Jengo la Rock City Mall jijini Mwanza kutokana na eneo hilo kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya Kamati hiyo aliwaomba wafanyabiashara wa madini kutoka mikoa jirani kama vile Mara, Shinyanga, Geita pamoja na Simiyu wakubaliane na walipokee bila kinyongo kwa kuwa lipo Mwanza litakuwa kitovu cha mikoa hiyo.
Waziri Nyongo alisema kuwa uanzishwaji wa soko hilo jijini, itakua njia moja wapo ya kujivunia na kutengeneza soko maarufu la madini ikiwa ni pamoja na kulitambulisha kimataifa.
Kwa Upande wake Rais wa Madini nchini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo John Bina alisema kuwa utafiti huo umebaini wanunuzi wa ndani wa madini hawana mitaji wengi wao ni madalali na kuiomba Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato (TRA) iwaangalie kwa kuweka kiwango rasmi cha kodi.
Rais Bina katika taarifa hiyo alisema kuwa kuanzishwa kwa soko hilo litaondoa utapeli kama vile kuuza na kununua dhaabu katika soko la madini kwani kuna wachimbaji wapo Dar es Salaam kazi yao ni kutengeneza dhahabu bandia na kulichafua Taifa letukatika mataifa mengine.
"Naomba Serikali katika sekta ya Madini kuhakikisha wanaanzisha mfumo maalumu utakaowatabua masonara wote nchini kwani wao ndio chanzo cha utoroshaji wa dhahabu kwenda nje ya nchi," alisisitiza.
Aidha alisema kuwa uchimbaji mdogo na wa Kati ni wa muhimu hasa katika ukuaji wa uchumi wa maendeleo ya Taifa kwani sekta hiyo ikiboreshwa itaongeza fursa za ajira kwa vijana.