Onyo upandishaji bei ya bidhaa Soko Kuu Pasaka

Na James Timber, Mwanza
Mwenyekiti wa Soko Kuu jijini Mwanza Bw. Ahmad Nchola, amepiga marufuku upandishaji wa bei ya bidhaa kiholela katika soko hilo kuelekea sikukuu ya Pasaka.

Akizungumza na Muungwana Blog Ofisini kwake amesema kuwa kumekuwepo na tabia kwa wafanyabiashara  juu ya upandishaji bei ya bidhaa katika soko hilo, ielekeapo misimu wa sikukuu hasa kwa vyakula vinavyopendeka zaidi na wengi kama vile mchele na viazi mviringo na kuku.

"Ni ukweli wafanyabiashara katika soko hili wamekuwa wanapandisha bei kwa bidhaa zinazopendeka kama vile kuku jambo linalowapa shida wateja wafikapo sokoni hapo nawaomba wafanyabiashara wajari wateja wetu", alisema Nchola.

Akizungumzia usalama wa soko amesema wameimarisha ulinzi na kuwataka wafanyabiashara wawe huru na mali zao ila kuna vibaka ambao wanaibia wateja na kuwataka wateja kuwa makini wafikapo katika soko hilo.

Pia amewataka wafanyabiashara wanaopanga bidhaa nje ya soko wawe wasafi watupe taka sehemu iliyotengwa kwa ajili ya taka, kwani wamekuwa wakitupa taka kwenye mitaro jambo linalosababisha  mitaro kujaa maji na kubadili mwelekeo kwa ajili ya uchafu unaoziba mitaro.

Aidha amesema changamoto kubwa ni utumiaji wa mashine za kielekitroniki zimekuwa zikiwachanganya na kuwachukulia muda mrefu kuzoea kwani hawakupata elimu juu ya utumiaji wa mashine hizo, ambapo ametaja bidhaa zinazoingia sokoni kwa wingi katika kipindi hiki kuwa ni Mahindi, Karanga na Kunde.
Mpya zaidi Nzee zaidi