Raia wa Urusi wapiga kura kumchagua rais

Raia nchini Urusi wameanza rasmi zoezi la kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa kumchagua rais mpya.

Takriban wapiga kura milioni 11 wanatarajiwa kushiriki katika zoezi hilo linalohusiaha wagombea nane

Raia wa Urusi milioni mbili wanatarajiwa kupiga kura wakiwa nje ya nchi yao.

Kwa mujibu wa habari,matokeo yaawali yameonyesha kuwa rais Vladimir Putin anaongoza kwani  asilimia 69 ya wananchi wako tayari kumpigia kura.

Paven Grudinin kutoka katika chama cha Party of Russian Federation anafuatia kwa asilimia 7.1.

Vladimir Zhirinovsky kutoka chama cha Liberal Democratic Party anafuatia kwa asilimia 5.6.

Zoezi la kupiga kura litamalizika siku ya Jumatatu 2.00 a.m saa za Moscow.

Putin anagombea kwa mara ya nne sasa.
Mpya zaidi Nzee zaidi