Klabu ya soka ya Singida United imekanusha taarifa zinazoeleza kwamba mshambuliaji wa timu hiyo Daniel Lyanga amefungiwa na Shirikisho la soka la Kimataifa FIFA na kueleza kuwa taarifa hizo sio kweli.
''Daniel Lyanga hajatungiwa miezi sita kucheza soka, Klabu yetu ya Singida United ilifuata taratibu zote za usajili na ulishirikisha pande zote mbili kati ya Fanja Fc na Singida United ikiwemo kulipa fidia za gharama za mkataba wake uliokuwa umebakia'', imeeleza taarifa ya klabu hiyo.
Singida United imeeleza kuwa kilichopo ni kuchelewa kwa hati ya uhamisho wa kimataifa ITC kutokana na dirisha la usajili hapa Tanzania kufungwa kitu ambacho sio mara ya kwanza kwa jambo hilo kutokea katika soka.

