Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Masoko wa Kampuni hiyo, Kabula Nshimo, amesema kuwa promosheni hiyo itahusisha watu walio juu ya miaka 18 na itakuwa siku ya Jumatano pekee.
Akifafanua, Nshimo alisema mtumiaji wa bia hiyo atakwenda kwenye vituo vya daladala/mabasi vyenye huduma hiyo ambayo kwa kuanzia wameanza na kituo cha Morocco na baadaye itasambaa vituo vingine vya daladala ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Kumbuka mashine hizo zitatoa bia kwa siku ya Jumatano pekee kuanzia saa 10 jioni hadi saa 6 usiku na washindi wote watapelekwa kwenye baa zilizo karibu na kituo husika.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

