TTCL washirikiana na tiGO kuzindua huduma ya kifedha (E-Money Joint Service)

1
Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL limeingia makubaliano ya ushirikiano wa biashara na kampuni  ya simu za mikononi ya Tigo yatakayowezesha wateja wa taasisi zote mbili kubadilishana fedha na huduma za fedha kupitia simu zao za mkononi.
Hayo yamesemwa na mkuu wa Huduma za TTCL pesa Bw.Moses Alphonce katika ghafla ya kutangaza ushirikiano huo nakusema kuwa kwa kushirikiana na tigo pesa katika kuwapa wananchi suluhisho sahihi la mahitaji yao ya kifedha ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi.
Aidha Bw.Alphonce  amesema TTCL imeazimia kuwapa wananchi huduma za kiwango cha juu na cha ubora na unafuu wa gharama za kutuma ,kupokea na kufanya miamala kwa kutumia simu Zao hivyo wamedhamiria kubadili mifumo ya malipo yote ya umma na binafsi yafanyike kupitia mtandao ili kuongeza usalama na ufanisi wa shughuli za kiuchumi na kijamii.
Kwa upande wake mkuu wa huduma za Tigo pesa Bw.Hussein Saidi amesema kuwa Tigo pesa imeazimia kufikisha huduma sehemu mbalimbali ambazo huduma za kifedha hazijafika ili kuwawezesha watu kufanya huduma za kifedha  kutoka tigo kwenda TTCL kwa kiwango kilekile.
4
Hata hivyo hatua hii ya makubaliano kati ya TTCL na Tigo ni muendelezo wa jitihada za shirika la mawasiliano Tanzania kurejea kwa kishindo katika soko la huduma za mawasiliano nchini  kwani hadi sasa TTCL imefanikiwa kufikisha huduma za 4G lite kutoka mikoa 16 ya Tanzania bara na Visiwa vya Pemba na Unguja
Mpya zaidi Nzee zaidi