Kampuni ya Tanzania Breweres Limited (TBL) kupitia kwa kinywaji cha Safari Lager imetangaza rasmi kuanzia Machi 21, 2018 promosheni ijulikanayo kama ''VUTA PUMZI KILA J’GWARA NA SAFARI NDOGO'' imeanza ambapo watumiaji wa bia ya safari lager watajishindia kinywaji hicho kwenye vituo vya daladala.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja wa Kampuni hiyo, Kabula Nshimo amesema kuwa promosheni hiyo itahusisha watu walio juu ya miaka 18 na itakuwa siku ya jumatano pekee ambapo itasambaa kwenye vituo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Aidha mtumiaji wa bia hiyo atakwenda kwenye vituo vya Daladala/Mabasi vyenye huduma hiyo ambayo kwa kuanzia Safari Lager wameanza na kituo cha Morocco ambapo washindi walioshinda wamepata zawadi ya bia kwenye bar ambayo ilichaguliwa kwenye kituo pia.
''Watuiaji na wateja wetu wa bia tumeamua kuwapa nafasi hii ili waweze kupata nafasi ikiwa ni moja ya fadhira ambazo tunawarudishia na wao wanufaike hivyo wafike kwenye vituo watakuta mashine na viti ambavyo vimeandikwa siku ambapo siku ya jumatano ndio fursa hiyo wataipata hivyo tunawaomba wateja wetu wafike kwenye kituo cha Mtongani kwa wiki ijayo" amesema Nshimo
Kumbuka mashine hizo zitatoa bia kwa siku ya Jumatano pekee kuanzia saaz 10 jioni hadi saa 6 usiku na washindi wote watapelekwa kwenye Bar zilizokaribu na kituo husika msikilize hapa chini Bi. Nshimo.