Waandishi wa habari wawili wa Ujerumani wakamatwa Ugiriki

Waandishi wa habari wawili wa Ujerumani wamekamatwa katika eneo la kijeshi nchini Ugiriki karibu na mpaka wa Uturuki.

Kwa mujibu wa habari,mwanamke mwenye umri wa miaka 31 na mwanamume mwenye umri wa miaka 33 wamekamatwa katika wilaya ya Didymoteicho kaskazinimashariki mwa Evros.

Wanahabari hao wa kituo cha televisheni cha ARD Ujerumani wamekamatwa baada ya kuingia katika eneo la usalama lisiloruhusiwa.

Walipohojiwa wamesema kuwa walikuwa wakiandika habari kuhusu waturuki wanaorudi Uturuki kutoka Ujerumani kwa kutumia njia zisizokuwa halali.
Mpya zaidi Nzee zaidi