Wahamiaji haramu 800 kutoka Afrika waachiwa Yemen

Wizara  ya  mambo ya ndani ya Yemen imetoa amri ya kuachiwa huru kwa wahamiaji haramu takriban 800 kutoka Afrika kusini mwa Aden.

Khaled al Ulvani,kiongozi wa idara ya wakimbizi na uhamiaji amekiambia kituo cha Anadolu kuwa waziri ametaka wahamiaji haramu kutoka Afrika ambao wamekamatwa Aden waachiwe huru.

Kwa mujibu wa habari,waziri ametaka shughuli zote katika kituo cha wakimbizi zisitishwe.

Hata hivyo ameonya kuwa kuna baadhi ya wakimbizi hao wameathirika na Ukimwi huku wengine wakishukiwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi ya Daesh na Al Qaeda.

Kuachiwa kwa wakimbizi kama hao kunaweza kuleta madhara kwa jamii.
Mpya zaidi Nzee zaidi