Na.Ahmad Mmow.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, Christopher Ngubiagai amewataka wakuu wa idara kusimamia,kutekeleza na kufuatilia kwa karibu yanayojiri katika idara zao ili kuepuka changamoto zinazotokana na utendaji na uwajibikaji mbovu.
Ngubiagai ametoa agizo hilo alipotembelea shule ya msingi Mtanga iliyopo katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.Ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi katika eneo hilo la utawala analoongoza.
Mkuu huyo wawilaya ambae alitoa agizo hilo baada ya kuziona na kusikia changamoto mbalimbali zilizopo katika shule hiyo ya watu wenye mahitaji maalumu,alisema umefika wakati kwa watendaji kusimamia,kutekeleza na kufuatilia karibu changamoto zilizopo ndani ya idara au maeneo wanayoongoza.Kwasababu baadhi ya changamoto zinatokana nakukosa usimamizi mzuri na wakaribu.
Alisema baadhi ya changamoto zilizopo kwa wananchi zinaweza kuondolewa na watendaji wa maeneo husika iwapo wakuu wa idara wangekuwa wanafuatulia kwa karibu.Hata hivyo baadhi yao hawafuatilii.Hivyo kuwa sehemu ya tatizo badala ya kuwa watatuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi.
Katika hali iliyoonesha mkuu huyo wa wilaya alitaka agizo lake hilo lianze kufanyiwa kazi kwa vitendo na haraka amewataka wakuu wa idara za elimu ya msingi,maendeleo ya jamii na mipango za halmashauri hiyo waeleze njia zitakazosababisha baadhi ya changamoto zilizopo katika shule hiyo zinatatuliwa haraka.
"Kila mmoja afahamu nakutenda kwa vitendo yale anayotakiwa kufanya katika idara anayoongoza.Niwakati wakushugulikia matatizo ya tunaowaongoza ili wafike kwenye maendeleo.Vinginevyo sisi tunaweza kugeuka nakuwa matatizo yenyewe,"alisema Ngubiagai.
Mbali na kutoa agizo hilo kwa watumishi wa umma,mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wilayani humo kushirikiana na serikali katika kujiletea maendeleo.Ikiwamo moyo wakujitolea na kusaidia kutatua kero zilizopo katika miradi ya maendeleo na huduma za jamii katika maeneo yao.
Miongoni mwa changamoto zilizopo katika shule hiyo ya Mtanga yenye wanafunzi 59 ni maji,vitabu vya kujifunzia na baiskeli kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa miguu.
