Korea Kaskazini yaongezewa vikwazo na EU

Umoja wa Ulaya umeongeza vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia majaribio ya makombora ya nyuklia ambayo yamekuwa yakifanywa na nchi hiyo.

EU imechukua hatua mpya za vikwazo kulingana na maamuzi ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Taarifa hiyo imetolewa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa habari,Umoja wa Ulaya una vikwazo vyake yenyewe dhidi ya Korea Kaskazini mbali na vile vilivyotajwa an Umoja wa Mataifa.

Umoja wa Ulaya pia imekataza kuingia kwa meli 15 katika bandari zake.

Umiliki wa makombora ya nyuklia na Korea Kaskazini umeonekana kuwa tishio kubwa kwa amani ulimwenguni.
Mpya zaidi Nzee zaidi