Makabiliano baina ya waandamanaji na Polisi katika miji tofuati nchini Ufaransa

Makabiliano  yaripotiwa kutokea katika miji tofauti nchini Ufaransa baina ya waandamanaji na jeshi la Polisi.

Maandamano yanaripotiwa katika miji tofauti nchini Ufaransa ambapo  raia wamemiminika mabarabarani  kupinga  mwenendo wa wa kisiasa wa serikali .  Maandamano yameripotiwa kufanyika mjini Nantes na Marseille.

Taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Ufaransa zimearifu kuwa makundi ya wanafunzi na  makundi ya walinda mazingira yameandamana kupinga serikali katika miji tofauti nchini Ufaransa.

Watu zaidi ya 100 000 wameandamana  kupinga kuaondolewa katika eneo ambalo kunatarajiwa kuanza ujenzi Notre-Dame-Des-Landes.
Mpya zaidi Nzee zaidi