Ndugu wananchi,
Tunapenda kuwashukuru sana kwa mapenzi yenu ya dhati kwa kuiamini Muungwana blog na Tv, tunawashukuru kwa kuendelea kutuamini na kutupa ridhaa ya kuendelea kuwapasha habari motomoto za Kisiasa, Uchumi, Burudani, Michezo na Makala mbalimbali ili kuendeleza gurudumu la nchi yetu ya Tanzania.
Muungwana blog na TV ni moja ya blogu ambayo imeanzishwa kwa ajili ya wananchi kupata habari zenye ubora, ukweli na uhakika ndani na nje ya nchi kwa ujumla, imani yetu mnaiamini na kuithamini blogu yenu ndio maana mpaka leo tunaendelea kusimama katika ubora wa utoaji wa huduma hii.
Kwa ujumla leo tumetimiza miaka mitatu tukiwa kifua mbele katika tasnia hii ya habari kwa kuupasha umma habari na matukio yanayojili pande zote za dunia kila siku kadri inavyowezekana, hivyo hatuna budi kuwahakikishia kuendelea kusimama huku tukisimamia waredi wetu wa habari unaotuongoza tukifuata kanuni na sheria za habari zilizowekwa.
"Tunasema Ahsanteni sana kwa dhamira yenu ya dhati ya kutusapoti kila uchwao kwani bila nyie wasomaji na watazamaji Muungwana haiwezi kuwa, hivyo tunaahidi kuendelea kusimama na kuwapasha habari motomoto zilizoandaliwa, kuhaririwa na waandishi makini"
Muungwana blog na Tv hatutawaangusha katika kuwapasha habari zinazojili kila siku, hivyo tunajivunia sana kuwa fahari na moja ya chombo bora chenye kutoa habari sahihi kwa jamii nzima pia tunawashukuru wasomaji na watazamaji wetu kwa upendo na ushirikiano wenu usio na kikomo.
KARIBU NA ENDELEA KUWA NASI

