“Kama nitasema tubadili aina ya ushambuliaji wetu, wachezaji wangu wataniangalia na kusema hatuamini na anaogopa na hilo sitaki litokee, tunakwenda Anfield kushambulia kama kawaida” hiyo ni kauli ya Pep Gurdiola kuelekea pambano lao vs Liverpool.
Rekodi zinaonesha kama kuna kocha ambaye ni tatizo kubwa kwa Pep Gurdiola baasi ni Jurgen Klopp, Klopp ndio kocha ambaye anamuonea zaidi Gurdiola kwani vipigo vitano alivyompa ni vingi zaidi kuliko kocha yoyote duniani kuwahi kumpiga Pep.
Huu ni mchezo wa 11 kwa Liverpool msimu huu(ikiwemo mechi ya kufudhu) na katika mechi hizo wana michezo 10 ambayo hawajapoteza hata mchezo mmoja, wakiwa wameshinda sita na kati ya hiyo kuna clean sheets 5.
Anfield ni mahala pa kujidai kwa Liverpool katika michuano ya Ulaya, katika michezo yao 14 iliyopita ya Ulaya majogoo hao hawajawahi kufungwa Anfield na mara ya mwisho kupoteza hapo ilikuwa mwaka 2014 katika mchezo wao dhidi ya Real Madrid.
Liverpool pia ndio klabu ambayo inashikilia rekodi ya kufunga mabao mengi katika michuano ya Champions League, hadi sasa wamefunga 28 huku wakiifukuzia rekodi ya Manchester United ya timu ya Uingereza kufunga mabao mengi CL katika msimu mmoja (mabao 32).
Hii ni mara ya kwanza kwa timu hizi kukutana katika michuano ya bara la Ulaya, lakini wamekutana katika michezo 178 ya michuano mbali mbali huku Liverpool wakishinda michezo 87, wakipigwa 45 na kwenda suluhu 46.
Kama kuna mchezaji wa kuchungwa zaidi Liverpool katika Champions League baasi ni Roberto Firminho, uwezo wake katika michuano hii umekuwa hatari sana kwa timu pinzani kuliko mshambuliaji mwingine yeyote Livepool.
Hadi sasa Mbrazil huyu ameshafunga mabao 7 katika Champions League huku akiwa pia ana assist 3 na hii inamfanya kuhusika katika mabao 10 katika CL msimu huu, idadi ambayo ni CR7 pekee ndiye aliye juu yake.
Kwa Manchester City Kun Aguero anaendelea kuwa mwiba mchungu kwa mabeki, katika mchezo dhidi ya Everton alikuwa nje kwa kuwa alikuwa na majeraha lakini sasa yuko fiti, Kun amewafunga Liverpool mara 6 na kutoa assist 3 katika mara 18 walizokutana na Liverpool.