Musiba amekanusha tuhuma hizo kwa kusema kwamba hajawai kusema atamuua mtu yeyote yule isipokuwa alisema kama angekuwa IGP wa nchi hii basi angemuweka mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, miaka 200 jela.
Aidha Musiba amesema Mbunge Selasini, alimuambia kuwa ana mpango wa kutoka Chadema na kuhamia CCM, na pia ameendelea kusisitiza kuwa Rais Magufuli na serikali iliyopo madarakani ni lazima iheshimiwe.
