Serikali inatarajia kuanzisha kampeni maalum itakayojulikana kwa jina la JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA yenye lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na ukosefu wa huduma bora za uzazi kwa wanawake pindi wanapojifungua.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya taasisi ya Child Survival International CSI ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.
Amesema takwimu za sasa zinaonesha vifo hivyo vimeongezeka na kufikia 536 kwa mwaka ambapo miongoni mwa hatua za kupunguza hali hiyo ni kuongezwa kwa bajeti ya afya na kufikia shilingi trilioni 1 ikijumlisha na michango ya wahisani huku kwa upande wake Rais mstaafu Jakaya Kikwete akitoa wito kwa wadau wa afya kushikamana na serikali ili kupunguza vifo hivyo.
Kwa upande wake mwanzilishi wa taasisi ya CSI Stella Mpanda amesema kwa miaka mitano wametoa mafunzo kwenye makundi mbalimbali akinamama na vijana wakike na wakiume ili kufahamu namna bora ya kufuata uzazi wa mpango ili kuepukana na vifo vya uzazi