NGOMA kukosa Mashindano ya Kagame CUP sababu Hizi Hapa


Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Afisa Habari wake, Jaffer Idd Maganga, umesema kuwa mchezaji wake aliyesajiliwa kutoka Yanga atakosekana dimbani kwa muda wa miezi miwili.

Maganga ameeleza hayo mara baada ya mchezaji huyo kuwasili leo nchini akitokea Afrika Kusini baada ya kufanyiwa vipimo vya afya katika hospitali ya St, Vincent Parrot iliyoko Cape Town.

Afisa Habari huyo amesema kuwa, kwa mujibu wa taarifa za Daktari, Mwanandi Mwankemwa, ameeleza kwamba Ngoma amegundulika kuwa na tatizo la uvimbe katika goti lake la kulia.

Mwankemwa amefafanua kuwa goti hilo limeonekana kuwa na uvimbe kwa ndani ambao ulikuwa unaelekea kupona hivyo itampasa afanye mazoezi mepesi kwa ajili ya kuliweka sawa na hatimaye aweze kupona vizuri.

Kutokana na hali hiyo, Maganga amesema Ngoma atapaswa kupumzika kwa muda wa miezi miwili na wiki moja na sasa atakayokosa mashindano ya Kagame CUP yanayotarajia kuanza mwisho wa mwezi huu.
Mpya zaidi Nzee zaidi