Serikali yaonya mamluki UMISSETA

Na James Timber, Mwanza
Serikali imewataka Viongozi wa Michezo UMISSETA na  Afisa Elimu Mikoa kuhakikisha wanafunzi wanaoshiriki michezo hiyo siyo mamluki.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa katika hotuba yake kwenye uzinduzi wa UMISSETA Kitaifa mkoani Mwanza, amesema walimu wahakikishe mshiriki anayeletwa kwa ajili ya michezo hiyo ni mwanafunzi anayetambulika kwani ndio nafasi pekee ya kuonesha kipaji alichonacho.

"Haturuhusu kushirikisha vijana ambao sio wanafunzi kwani siyo nafasi yao na ambapo tutabainisha udanganyifu tutachukua hatua kwa huo mkoa ambao umefanya vitendo hivyo," alisema.

Pia Majaliwa amesema kuwa pamoja na manufaa yatokanayo na michezo ila bado kiwango cha michezo nchini kimeporomoka, ambapo dawa ni kupeleka walimu wa michezo wenye taaluma hiyo kuanzia ngazi za awali.

 Aidha amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dk. John Magufuli katika juhudi za kuunga mkono michezo, anazitaka halmashauri zote kutenga fedha kupitia Baraza la Madiwani lengo likiwa kukusanya fedha na kugawa vifaa vya michezo kuanzia shule za awali hadi vyuo vya michezo.


Mpya zaidi Nzee zaidi