F Spika Ndugai ashuhudia alichokifanya Mbunge Mariamu ampongeza | Muungwana BLOG

Spika Ndugai ashuhudia alichokifanya Mbunge Mariamu ampongeza


Spika wa Bunge Job Ndugai ameshuhudia wana CCM jijini Dodoma wakikabidhiwa kompyuta 25 na printa zake kwa wanajumuia wa chama  ngazi ya Mkoa na wilaya na jumuia zake tatu ikiwa ni utekerezaji wa majukumu ya ilani na ahadi ya Mbunge Mariamu Ditopile.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo Spika Ndugai amemsifu na kumpongeza Mbunge Mariamu kwa kuthubutu kutekeleza ahadi hiyo kwani kuna viongozi wengi hawawezi kutekeleza vitu wanavyoahidi.

"Leo nimeshuhudia maajabu ambayo sijawahi kuyaona kwa wabunge wa Viti maalumu huyu mbunge ni mfano wa kuigwa sana kwa wana CCM wote nchini kwani kwasasa  tunakoelekea Tanzania hatupiga tena kampeni kwenye majukwaa tutatumia mitandao ya kijanii kuomba kura hivyo lazima tujiandaa" amesema Spika Ndugai.

Mariamu Ditopile namfahamu vizuri sana huyu ni mkulima na anapambana sana kwenye kilimo kwanini tusimuige, kila kijana na mwana CCM lazima aige mifano mizuri kama hii aliongeza Spika ndugai.

Kwa upande wake Mariamu Ditopile amesema  amekabidhi vifaa hivyo vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 25 lengo likiwa ni kuendelea kurahisisha shughuli za chama ambazo zinalenga kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi.

" kama tunavyofahamu chama ni ofisi hivyo vifaa hivi vitarahisha kazi na majukumu ya chama kama vile kuchapisha majalada kuhifadhi data katika jumuia zetu ngazi Mkoa na wilaya" amesema Mariamu.

Aidha ameongeza kuwa ili CCM isonge mbele lazima iwe na vitendea kazi ambavyo vinaendana na wakati na kurshisisha kazi ili kufikia  malengo ya chama.

Pia kutokana na yeye kuwa mkulima ameahidi kutoa majembe 500 kwa kila halmashauli ili kuinua sekta ya kilimo nchini hususani kwa vijana ambao wanalalamika kuwa hawana hawana ajira hivyo hawana budi kuchangamkia fursa hii.