Navy Kenzo waweka wazi sababu ya kufanikiwa kufanya kazi na Diamond na Alikiba pamoja



Unafahamu sababu za Navy Kenzo kuweza kufanya kazi na Diamond na Alikiba huku wasanii hao wawili wakiwa wanaonekana kuwa na bifu la kufa mtu?

Wakiongea na kipindi cha Chill na Sky cha Dizzim Online, Aika na Nahreel wamesema sababu hiyo ya kuweza kufanya kazi na wasanii hao wamekuwa wakijiweka mbali na team zao na kufanya muziki wao ndio uwatambulishe zaidi kuliko kuingilia ugomvi wa watu wengine. 

"Tunajaribu kufanya umaarufu wetu ujengwe na muziki, Mimi na Aika tunataka watu watukumbuke kupitia muziki na sio wale ndio waliingilia bifu fulani. Tunapenda kuishi maisha mazuri hatupendi kuwa na stress za ugomvi au maneno," wamesema wasanii hao.

Tayari kuna ngoma kubwa wameshafanya na Diamond japo hajataka kuzungumzia kama wimbo huo wa Navy Kenzo au utakuwa wa Diamond.


Mpya zaidi Nzee zaidi