TARURA kuja na mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato kwa Wananchi

TARURA KUJA NA MFUMO MPYA WA KUEGESHA MAGARI NA UKUSANYAJI WA MAPATO KWA WANANCHI

Na Paschal D.Lucas, Mwanza

Katika kuboresha huduma za maegesho ya magari  na ukusanyaji wa mapato kwa mfumo mpya  katika jiji la Mwanza,wakala wa barabara za mjini na vijijini Tanzania (TARURA) kwa kushirikiana na shirika la NPK kutoka nchini Uholanzi leo Julai 20,2018 imetambulisha mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato kwa njia za kielektroniki jijini Mwanza.

Akitambulisha mfumo huo Mratibu wa TARURA mkoa wa Mwanza Eng.Koyoya Fuko  amesema mfumo huo utasaidia kukusanya zaidi mapato kuliko ilivyo sasa ambapo kupitia mfumo huo wa kisasa hakutakuwa na mtu yeyote atakayepokea pesa bali pesa hiyo italipwa kwa njia ya simu na vibanda vichache sana ili kumsaidia mwanachi aliyeko nyumbani kutambua na kufahamu sehemu iliyowazi kwa ajili ya kuegesha gari lake kabla hata yakufika mjini kwa kupitia simu au kompyuta yake na hivyo anaweza kulipia na kuja kuegesha gari lake bila tatizo lolote.

"Wananchi wataelimishwa namna gani wanaweza kutumia pakini za jiji la Mwanza hata wakiwa nyumbani kabla hajaja mjini anauliza ni sehemu gani katika jiji la Mwanza sasa hivi kuna pakini nataka kwenda sehemu fulani, kwa hiyo analetewa option za online na yeye atachague eneo analotaka kwenda kupaki na kufanya shughuli zake" Alisema Eng. Fuko.

Aidha akizungumzia vifaa vitakavyofungwa amesema kuwa baada ya mfumo kuwekwa kutakuwepo na kamera maalumu vitafungwa kwenye baadhi ya miradi, pikipiki zinazotumia umeme na kutakuwepo na sehemu maalumu (Dispass center) ambapo takwimu za taarifa zote za barabarani  zitakuwa zinapokelewa hapo.

Katika kutoa elimu juu ya mfumo huo mpya kwa Wananchi TARURA watatoa somo baada ya kufunga mfumo huo mpya kwa muda wa miezi mitatu kabla ya kuanza kufanya kazi rasmi kwa njia ya Luninga na kuwatembelea wananchi katika kata zao ili kurahisisha uelewa wa utumiaji wa mfumo huo.
Mpya zaidi Nzee zaidi