Juventus wampoteza mkongwe mwingine baada ya Buffon na Lichtsteiner


Mchezaji mkongwe wa klabu ya soka ya Juventus, Claudio Marchisio, ameachana na klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 25.

Taarifa rasmi zimeeleza kuwa Marchisio na Juventus wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wao ambao ulikuwa unaisha mwaka 2020.

Mchezaji huyo ameitumikia Juve katika mechi 389 huku akishinda makombe saba ya ligi k ya Italia na Bianconeri, na makombe manne ya Coppa Italia.

Marchisio alipata majeraha makubwa ya goti mwaka 2016 yaliyomuweka nje kwa miezi 6, msimu uliopita alifanikiwa kucheza mechi 20.

Msim huu Juve wamewapoteza wachezaji wao wakongwe Gianluigi "Gigi" Buffon aliyetimkia (PSG), Lichtsteiner aliyesajiliwa (Arsenal).
Mpya zaidi Nzee zaidi