Rais wa Liberia George Weah ampataia tuzo kubwa Arsene Wenger


Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ametunukiwa tuzo ya hadhi ya juu zaidi nchini Liberia.

Mzee Wenger ametunukiwa tuzo hiyo inayofahamika kama "The Knight Grand Commander of the Humane Order of African Redemption" na rais wa nchi hiyo George Weah.


Arsene Wenger ndiye aliyemsajili Weah kipindi anaifundisha klabu ya Monaco mwaka 1988. 

Imeelezwa kuwa Arsene Wenger kapewa tuzo hiyo kutokana na mchango wake wa soka barani Afrika, pamoja na kuwapa nafasi waafrika wengi kipindi anafundisha.

Kocha mwingine ambaye amepewa tuzo na Weah ni Claude LeRoy, raia wa Ufaransa ambaye pia ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya Togo.
Mpya zaidi Nzee zaidi