Naibu waziri wa elimu mafunzo ya ufundi William Olle Nasha amewataka wadau wa sekta ya elimu wakiwemo wadhibiti na wakaguzi kuacha kutumia changamoto zilizopo kuwabebesha walimu mzigo wa lawama badala yake wasaidiane nao kuzitatua.
Akizungumza na wadhibiti wa viwango vya elimu wa mkoa ya kanda ya kaskazin Olle Nasha amesema baadhi ya watendaji wa sekta hiyo wakiwemo wakaguzi wamekuwa wakikimbilia kukagua mapungufu tu na kuwaachia walimu kana kwamba wao hawahusiki na kwamba wanaofanya hivyo watawajibishwa.
Mdhibiti wa ubora wa shule kutoka wizara ya elimu Agusta Mpokela pamoja na kukiri kuwepo kwa changamoto amesema zinaendelea kushughulikiwa na kupungua baada ya kuanza kutumka kwa mfumo mpya elimu.
Olle Nasha pia ametembelea na kukagua karakana ya chuo cha ufundi Arusha na kueleza kuwa serikali inaendelea kuviboresha na kuviimarisha kwa kuweka vifaa , mashine na zana za kisasa za kufundishia.
Baadhi ya watendaji wa vyuo vya ufundi wamesema pamoja na serikali kutumia mabilioni ya fedhakuwekeza katika vifaa vya kisasa kuna changamoto kubwa ya uwezo mdogo wa wanafunzi wanajiunga na vyuo hivyo.
