Watuhumiwa sugu 13 wanaswa na Polisi Dar


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia watuhumiwa sugu 13 kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji na mikoa ya jirani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 17 Kamanda wa Polisi kanda Maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa amewataja watuhumiwa hao kuwa  ni Balizanila Ezekiel  (37) raia wa Burundi, Shukuru Hassan(38), Shaibu Shaban (34) Haji Salum (38) Frenk Kalikene  (32) na wengine 8.

Kamanda Mambosasa ameongeza kuwa watuhumiwa hao wamekuwa wakiendelea na vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha licha ya kuachiwa huru baada ya kumaliza vifungo vyao katika magereza mbalimbali hapa nchini.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na bostola aina ya Chinese star iliyokuwa na risasi nne ndani ya magazine, pamoja na risasi nyingine tisa zikiwa zimehifadhiwa pembeni.

Oparesheni hii ni endelevu ya kupambana na wahalifu wote wanaofanya unyang’anyi ndani ya jiji la Dar es salaam na wanaokuja kujificha jijini Dar es salaam baada ya kufanya uhalifu kutoka mikoa ya jirani.

Mpya zaidi Nzee zaidi