Zaidi ya Shilingi Milioni 560 zimetengwa katika ujenzi wa zahanati



Na James Timber, Mwanza

Jumla ya fedha shilingi milioni 561 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati kwenye Kata Tano zilizopo katika Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza.

Akizungumza na Vyombo vya Habari katika Ziara yake ya kukagua ujenzi wa Zahanati katika Jimbo hilo Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula alisema kuwa lengo kubwa ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwasogezea huduma hiyo karibu tofauti na hapo awali walipokuwa wakiifuata umbali mrefu.

Mabula alibainisha  kata zilizopata fedha hizo kuwa ni pamoja  na Isamilo shilingi  milioni 107, Bugarika shilingi milioni 67, Mahina  shilingi milioni 87  na Kata za Mhandu na Mkuyuni zilizopokea kiasi cha shilingi milioni 150 kila kata.

Aidha Mbunge huyo alifafanua chanzo cha fedha hizo kuwa ni kutokana na makusanyo ya ndani ya mapato huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza James Bwire kwa kuwa kipaumbele katika kuboresha sekta ya afya katika Jiji hilo.
Mpya zaidi Nzee zaidi